Kaimu Mganga Mkuu wa hospitali ya wilaya ya Kisarawe Dkt. Zaitun Hamza
EATV imefika ofisini kwa Kaimu Mganga Mkuu wa hospitali ya wilaya ya Kisarawe Dkt. Zaitun Hamza, ili kupata undani wa sakata hilo na kusema kuwa taarifa hizo hazina ukweli wowote kwani taarifa hiyo ilianza kuzagaa mitandaoni Agosti 21, 2022, ili hali mgonjwa alifanyiwa upasuaji Agosti 18, mwaka huu.
Mganga Mkuu huyo amesema mgonjwa alifika hospitalini hapo Agosti 14, akiwa na hernia na akafanyiwa matibabu ya awali kisha akaruhusiwa na kupewa taratibu zote kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji na kwamba alitakiwa alipie gharama ya upasuaji ambayo ni shilingi elfu 50 tu na si shilingi laki mbili na hamsini iliyoripotiwa kwnye mitandao hiyo ya kijamii.


