Mkurugenzi wa taasisi hiyo Dkt Respicius Bonifasi akizungumza na waandishi wa habari amesema upasuaji huo ulioanza unafanyika kwa ushirikiano na jopo la madaktari kutoka India ambapo wagonjwa watafanyiwa upasuaji huo bila kufungua fuvu la kichwa
Kwa upande wake daktari bingwa wa upasuaji wa ubongo pamoja na mishipa ya fahanu Dkt Laurent Mchome amesema kila siku Noi inapokea wagonjwa si chini ya watatu ambao Wana tatizo la kupooza zinazosababishwa na Damu kuvilia ndani ya ubongo na kuongeza kuwa tatIzo Hilo ni kubwa kwenye jamii
Naye mwakilishi Wa jopo la madaktari kutoka nchini India amesema upasuaji huo wa ubongo kati Yao na nadaktari wa MOI ni muendelezo wa ushirikiano baada ya kuingia makubaliano hayo has kwenye nyanja ya upasuaji ubongo na mishipa ya fahanu na magojwa yanayohusiana na UTI Wa mgongo
