Ijumaa , 7th Oct , 2022

Naibu waziri wa mifugo na uvuvi Abdallah Ulega ameitaka mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira DAWASA mkoani Pwani kuhakikisha wanatenganisha vyanzo vya maji na malisho ya wanyama vilivyopo karibu na mapitio ya mifugo

Lengo ni kuzuia uharibifu wa vyanzo vya maji katika mto Ruvu ikiwa ni pamoja na kuepusha migogoro inayoweza kujitokeza.

Akizungumza wakati wa kukagua mabanda ya biashara ikiwa ni siku ya pili ya maadhimisho ya wiki ya wawekezaji wa viwanda na biashara mkoani Pwani waziri ULEGA amesema kumekuwapo na uharibifu mkubwa wa vyanzo vya maji unaosababishwa na mifugo ambayo hupitishwa pindi wanapopelekwa malishoni.

Katika maonesho hayo ya tatu kufanyika mkoani hapa tukashuhudia shughuli mbalimbali za uzalishaji mali zikiwemo rasilimali zinazopatikana mkoani Pwani.