
Baadhi ya maafisa wa polisi wakiwa na mwili walioufukua
Tukio la kufukua mwili huo limefanyika hii leo Oktoba 12, 2022, katika eneo la Kijiji cha Mbigili Kata ya Partimbo mkoani Manyara, na kwamba mwili huo umekutwa ukiwa umeharibika vibaya tena ukiwa umezungushiwa mfuko wa salfeti mithili ya sanda na kufukiwa pembeni mwa barabara itokayo kijiji cha Mbigili kuelekea Kiteto.
Mabaki ya mwili huo wa marehemu uliofukuliwa yamehifadhiwa chumba cha maiti katika hospitali ya wilaya ya Kiteto huku ikielezwa kuwa uchunguzi zaidi wa Polisi unaendelea kutambua mwili huo.