Mkurugenzi Mtendaji wa Moi Dkt Respicious Boniphace,
ambao umewafanya watu wengi kukutana na shida katika mishipa ya damu iliyopo kichwani.
Hayo yameelezwa leo jijini Dar es Salaam wakati wa kambi ya mafunzo kwa wataalamu wa upasuaji wa ubongo kutoka Moi ambapo akizungumza Mkurugenzi Mtendaji wa Moi Dkt Respicious Boniphace, amesema katika kambi hiyo tayari wagonjwa wanne wameshafanyiwa upasuaji kupitia vifaa vya kisasa chini ya mtaalamu wa upasuaji kutoka nchini Ugiriki ambaye amekuwa akiendesha kambi hiyo ya mafunzo.
Kwa upande wake mkufunzi na mtaalamu mbobezi wa upasuaji wa mishipa ya damu kwenye ubongo Profesa Athanios Petridis, pamoja na daktari bingwa mbobezi wa upasuaji wa ubongo kutoka Moi Dkt Nice Phorus Rutasibwa, wamesema katika kambi hiyo wanatarajiwa kuongeza uwezo kwa madaktari wa Moi ambao kwa sasa wapo 13 ili kupata wataalamu wengi watakaosaidia katika upasuaji wa mishipa ya damu kwenye ubongo matatizo ambayo kwa sasa yameongezeka .
Kambi hiyo ni ya siku saba ambapo tayari wagonjwa wanne wameshatibiwa kati ya wagonjwa 7 wenye kupooza huku baada ya kambi hiyo kukamikika kutawezesha Moi kuweza kuhudumia wagonjwa 40 kwa mwaka huu kupitia teknolojia ya kisasa na vifaa vya kisasa ambavyo vitaweza kuziba mishipa ya damu kichwani iliyo pasuka .


