Ijumaa , 20th Jan , 2023

Mhandisi wa usafirishaji umeme mkoa wa Mwanza na Mara Shakiru Abdallah, amesema kwamba kijana aliyepanda juu ya nguzo ya umeme wa msongo wa kilovoti 132 kwenye njia ya Mwanza- Musoma, anakabiliwa na changamoto za matatizo ya afya ya akili.

Nzungu Ndaki, alivyokuwa amepanda juu ya nguzo ya umeme

Kijana huyo Nzungu Ndaki anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 25 hadi 30, alifanya tukio hilo jana Januari 19, 2023, na kwamba kwa mujibu wa shemeji yake kijana huyo alikuwa akipatiwa matibabu ya kienyeji.

Akizungumza na East Africa TV & EA Radio Digital, Mhandisi Shakiru, amesema kuwa hata hivyo zoezi la kumshusha lilifanikiwa baada ya kupata kibali cha kuzima umeme kwa muda, na kwamba alikabidhiwa kwa mamlaka za Jeshi la Polisi mkoani Mara.