Yanga yainyuka Coastal bao 2-0 Mkwakwani
Klabu ya Yanga imeendelea kujikita kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Coastal Union, na sasa kikosi hicho cha timu ya wananchi kinaongoza Ligi kwa tofauti ya alama 8. Huu ni ushindi wa kwanza kwa Yanga mkoani Tanga baada ya miaka 6.