Magari yakwamba Bukoba ubovu wa barabara
Magari yanayosafiri kutoka Bukoba mkoani Kagera kuelekea mikoa mingine, yamekwama katika eneo la Kyetema kufuatia kuharibika kwa barabara ya dharura inayotumiwa na magari hayo na kusababisha adha kwa abiria huku ikielezwa kuwa uharibifu huo umetokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha.