Timu ya Chelsea ya Wanawake yatwaa ubingwa WSL
Mabingwa wa ligi kuu ya wanawake England Chelsea wamekuwa timu ya kwanza ya wanawake kumaliza msimu bila kufungwa baada ya hii leo kushinda 1-0 dhidi ya Liverpool na kukabidhiwa kombe mbele ya mashabiki wao kwenye dimba la Stamford Bridge .