
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli.
Katibu Mkuu huyo wa CCM ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na viongozi wa chama hicho mkoa wa Geita ambapo pia aliwaagiza viongozi wake kufanya siasa safi kwa ajili kuwaunganisha wananchi na si kuleta mvuragano baina ya serikali na wananchi hao.
Aidha Dkt. Bashiru amesema anawaonya wenye nia ya kupata ubunge na kuudharau uteuzi waliopewa na Rais Magufuli, na kudai kuwa amepewa taarifa kuna baadhi ya wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya kukimbilia majimboni.
Hivi karibuni Katibu Mkuu huyo alimualika kiongozi wa Chama Cha ACT na Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini Zitto Kabwe.
''Nampongeza kiongozi wa ACT-Wazalendo ndugu Zitto Kabwe kwa kuibua mijadala mbalimbali ya kiuchumi, nimtake na kumkaribisha ajiunge na CCM, chama cha ujamaa wa kweli","alisema Dkt Bashiru.