Dkt Kikwete akisaini kitabu cha maombolezo
Rais mstaafu Kikwete, leo akiambatana na mkewe Mama Salma Kikwete, amesaini kitabu cha maombolezo katika ubalozi wa Kenya jijini Dar es salaam, kufuatia kifo cha mke wa Rais mstaafu wa Kenya Mwai Kibaki, Mama Lucy Kibaki kilichotokea juma lililopita nchini Uingereza.
Rais mstaafu Jakaya Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wamepokelewa ubalozini hapo na naibu balozi wa Kenya nchini Tanzania balozi Boniphace Muhia.
Rais mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete anatarajiwa kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, kwenye maziko ya Mama Lucy Kibaki yanayotarajiwa kufanyika huko Othaya kaunti ya Nyeri, nchini Kenya Jumamosi ya May 07, 2016.