Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Mabilioni yaliyotumika na serikali kwenye korosho

Monday , 10th Dec , 2018

Serikali imesema mpaka sasa imelipa zaidi ya shilingi bilioni 83 kwa wakulima wa korosho katika mikoa ya Lindi, Mtwara, pamoja na Ruvuma huku zaidi ya wakulima 82,835 kutoka mikoa hiyo wakiwa wamepatiwa fedha zao.

Korosho

Kwa mujibu wa Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga Jumla ya fedha iliyolipwa kwa wakulima hao ambao tayari wamefanyiwa uhakiki katika Mkoa wa Mtwara pekee ni 50,835, Lindi wakulima 22,131 na Mkoa wa Ruvuma ambao takribani wakulima 9,445 wamelipwa.

Akizungumza kwenye mkutano wa wabanguaji wadogo wa korosho wa mikoa mitano ya Mtwara, Lindi, Ruvuma, Pwani na Morogoro, Waziri Hasunga amesema jumla ya vyama 328 vimefanyiwa uhakiki ambapo kati ya vyama 504 vilivyopo katika mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma, jumla ya vyama 319 vimekwishalipwa.

Waziri Hasunga amesema kuwa kikao hicho kina lengo la kujadiliana na kukubaliana utaratibu uliopangwa na serikali katika ubanguaji wa korosho mwaka 2018/2019 kwa kuelekeza ubanguaji kufanyika nchini ili kuwanufaisha wananchi katika ajira hiyo.

Tumeiona changamoto ya mitaji kwa wabanguaji wadogo nchini sambamba na wabanguaji wakubwa hivyo ili serikali iwarahisishie upatikanaji wa mitaji tumeamua kuwapa kazi nyinyi wenyewe,” amesema Japhet Hasunga.

Aliongeza kuwa swala la uhakiki limejikita zaidi kubaini udanganyifu unaofanywa na baadhi ya wahujumu wa biashara ya korosho, “kuna watu walikuwa wametoa akaunti za benki lakini zinatofautiana na majina ya watu waliowasilisha korosho zao kwenye maghala ya kuhifadhia”.

Tulipoona soko la korosho linayumba huku lengo la serikali likiwa ni kutaka kuonana wakulima wananufaika tuliamua kuingilia kati na kuanza kununua korosho zote na kwa kwenda mbele zaidi tumeamua kubangua korosho zote hapa hapa nchini”.
 

HABARI ZAIDI

DCP David Misime, Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania

Mtoto atekwa na mzazi wake ili ajipatie milioni 20

Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Anton Sabasaba Akizungumza wakati alipohudhuria kikao cha wazazi katika Shule ya Msingi Elisabane Mei 24, 2024

Wototo wafuatiliwe na kulindwa kama mboni - Anton

Maduka ya Wafanyabiashara yakiwa yamefungwa

Wamiliki wa maduka Mebya wafunga biashara zao

Kamanda wa Polisi mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Agustino Senga

Polisi waambiwa kazi yao ni kazi ya Mungu

Kiwanda cha sukari Mtibwa

11 wafariki dunia kiwanda cha Mtibwa

Wilman Kapenjama Ndile, Mkuu wa Wilaya ya Songea

DC Kapenjama ataka uaminifu kwa wakulima Songea

Bashiri Mohamed (35) Mwenye Koti Jeusi akiwa anafikishwa Mahakamani Ilemela, Jijini Mwanza

Aliyezini na binti yake apandishwa kizimbani