Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Mahakama kuamua matumaini ya CUF

Wednesday , 18th Jul , 2018

Mbunge wa Temeke, Abdallah Mtolea ameweka wazi kwamba anaamini chama chao kitasimama tena upya licha ya changamoto na migogoro inayoendelea ambayo kwa kiasi kikubwa imeleta mpasuko mkubwa ndani ya chama.

Mbunge wa Temeke, Abdallah Mtolea

Akizungumza na www.eatv.tv, Mtolea amesema kwamba bado anaamini meza ya mahakama inaweza kuwa suluhisho la migogoro ya Chama chao ambayo imedumu kwa takribani miaka mitatu sasa.

Mtolea ambaye ni Mbunge asiyemuunga mkono Prof. Ibrahim Lipumba amesema kwamba, anaamini vyama vingi vina migogoro, na kwamba  hakuna chama kisicho na migogoro kwa kuwa wanasiasa wanakuwa na mitazamo tofauti.

"Sisi tusiomtambua Prof. Lipumba kama Mwenyekiti wa CUF, tunaaamini zaidi kwenye utawala wa sheria tunaamini kwamba mahakama itatusaidia kumaliza mgogoro wetu na tutasimama kuwa wapya na  imara zaidi kama awali. Kwa sasa siwezi kutoa maamuzi ya kwamba upande flani utashinda au utashindwa ila kesi zilizopo mahakamani ndizo zitakazoamua hatima ya chama chetu. Matatizo ni sehemu ya changamoto kwenye siasa Chama kisicho na migogoro kinaweza kuwa na watu wa ajabu sana. Tupo kwenye siasa kwa kuwa tunaamini tuna mawazo tofauti na maoni tofauti, hivyo kutofautina kwa mawazo hakujawahi kuwa mgogoro wa kudumu." Mtolea

Akizungumzia kuhusu mtu mmoja (Naibu Katibu Mkuu, Magdalena Sakaya) kuonekana kuwa na mamlaka ndani ya chama chao, Mtolea amesema hayo yote yanasababishwa na udhaifu wa serikali ndiyo maana mwanamama huyo anaonekana na nguvu.

"Siyo kwamba Sakaya ananguvu ya kukiendesha chama lakini serikali kwa kuwa ni dhaifu ndiyo maana inaonekana hivyo, kwa mfanoo kitendo cha Mkurugenzi kukubali kuvuliwa uanachama kwa madiwani wetu Tanga ni udhaifu kwani fika ilikuwa inafahamika kuwa chama kina matatizo na kesi takribani 13 zipo mahakamani" Mtolea

Chama cha CUF kilianza kuwa na mgogoro mwaka 2016 baada ya Mwenyekiti wao Prof. Ibrahim Lipumba kutangaza kurejea kwenye nafasi yake ya uongozi ambayo alijiuzulu wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
 

HABARI ZAIDI

DCP David Misime, Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania

Mtoto atekwa na mzazi wake ili ajipatie milioni 20

Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Anton Sabasaba Akizungumza wakati alipohudhuria kikao cha wazazi katika Shule ya Msingi Elisabane Mei 24, 2024

Wototo wafuatiliwe na kulindwa kama mboni - Anton

Maduka ya Wafanyabiashara yakiwa yamefungwa

Wamiliki wa maduka Mebya wafunga biashara zao

Kamanda wa Polisi mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Agustino Senga

Polisi waambiwa kazi yao ni kazi ya Mungu

Kiwanda cha sukari Mtibwa

11 wafariki dunia kiwanda cha Mtibwa

Wilman Kapenjama Ndile, Mkuu wa Wilaya ya Songea

DC Kapenjama ataka uaminifu kwa wakulima Songea

Bashiri Mohamed (35) Mwenye Koti Jeusi akiwa anafikishwa Mahakamani Ilemela, Jijini Mwanza

Aliyezini na binti yake apandishwa kizimbani