Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Miss wa gereza ahukumiwa Kifo

Thursday , 19th Jul , 2018

Mlimbwende wa taji la urembo katika gereza kuu la wanawake la Lang'ata (Miss Lang’ata Prison 2016)  Jijini Nairobi amehukumiwa kifo baada ya kukutwa na hatia ya kumuua mpenzi wake aliyefamika kwa jina la Farid Mohamed mwaka 2015.

Bi. Ruth Wanjiku Kamande (Miss Lang’ata Prison 2016.

Mrembo huyo mwenye jina la Ruth Wanjiku Kamande amepatikana na kosa la kumuua mpenzi wake huyo katika mtaa wa Buruburu, Nairobi mnamo tarehe 20 Septemba, 2015 baada ya kuwa na mvutano kati yao.

Jaji Jessie Lessit amesema upande wa mashtaka ulithibitisha kumkuta mshatikiwa na hatia pasipo kuwa na shaka yoyote ambapo amedai kwamba  vitendo vya Kamande vilionyesha aliua kwa kukusudia.  

Kwa mujibu wa vyombo vya habari kutoka Kenya vimeripoti kwamba mrembo huyo alijitetea kwamba mzozo kati yake na mpenzi wake ulikuja pale alipoiona kadi ya hospitali iliyoashiria kwamba Mohammed alikuwa akipokea matibabu ya Ukimwi. 

Aidha ameeleza kwamba mpenzi wake huyo (marehemu Mohamed) alimwambia wakati huo ni heri wafe wote kuliko hali yake ya Ukimwi ifahamike hadharani ambapo wakati mzozo ukiendelea ulimpelekea kumchoma na kisu kilichokuwa kinachotumiwa jikoni. 

Pamoja na hayo mahakama imekataa utetezi wa Bi Wanjiku wa kwamba marehemu alijaribu kumbaka ambapo ilielezwa kuwa uchunguzi wa madaktari ulionyesha hakukuwa na ukweli kuhusu madai hayo.

Wanjiku kwa sasa ambaye ana umri wa miaka 25 wakati anakamatwa ndiyo alikuwa amejiunga na Chuo Kikuu cha Kilimo na Teknolojia cha Jomo Kenyatta (JKUAT) kusomea masuala ya biashara, kwa mujibu wa wakili wake.

Wanjiku amekuwa mahabusu tangu mwaka 2015 katika gereza la Lang'ata  akisubiri maamuzi ya mahakama dhidi ya shtaka lake.
 

HABARI ZAIDI

DCP David Misime, Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania

Mtoto atekwa na mzazi wake ili ajipatie milioni 20

Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Anton Sabasaba Akizungumza wakati alipohudhuria kikao cha wazazi katika Shule ya Msingi Elisabane Mei 24, 2024

Wototo wafuatiliwe na kulindwa kama mboni - Anton

Maduka ya Wafanyabiashara yakiwa yamefungwa

Wamiliki wa maduka Mebya wafunga biashara zao

Kamanda wa Polisi mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Agustino Senga

Polisi waambiwa kazi yao ni kazi ya Mungu

Kiwanda cha sukari Mtibwa

11 wafariki dunia kiwanda cha Mtibwa

Wilman Kapenjama Ndile, Mkuu wa Wilaya ya Songea

DC Kapenjama ataka uaminifu kwa wakulima Songea

Bashiri Mohamed (35) Mwenye Koti Jeusi akiwa anafikishwa Mahakamani Ilemela, Jijini Mwanza

Aliyezini na binti yake apandishwa kizimbani