Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis akimuwekea mikono mmoja wa Makadinali aliowateua.
Papa Francis amechagua theluthi moja ya makadinali ambao watamchagua mrithi wake wakati Makadinali walio chini ya miaka 80 pekee ndiyo ambao wanaweza kumchagua Papa mpya ambapo makadinali 13 kati ya wale walioteuliwa wako chini ya miaka 80.
Hii ni mara ya tatu katika kipindi cha miaka mitatu ambapo Papa Francis, ambaye ni Papa wa kwanza kutoka Amerika ya Kusini kuwateua makadinali wapya ,Makadinali hao wapya wanatoka nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati , Bangladesh, Papua New Guinea na Mauriotius.

