Friday , 29th Apr , 2016

Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi a.ka. Sugu leo atashiriki mahojiano maalum katika kipindi cha Friday Night Live kinachorushwa na kituo cha EATV.

Sugu atafanyiwa 'exclusive interview' leo ikiwa ni kwa mara ya kwanza ndani ya miaka mitatu ambapo pamoja na mambo mengine atajibu maswali kuhusiana na wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la Freedom.

Katika hali ambayo inadaiwa na Mr. Blue kwamba ni kumzunguka katika wimbo huo wa Freedom ambapo Mr. Blue anadai kwamba wimbo ni wake alimshirikisha Sugu ila Sugu akaufanya mwenyewe, majibu ya Sugu kuhusiana Mr. Blue atafunguka ndani ya FNL leo.

Aidha wiki iliyopita watazamaji walifurahia kuzinduliwa kwa video ya Lady JayDee inayokwenda kwa jina la NdiNdiNdi na leo watamsikia Sugu live akielezea kuhusu wimbo wake wa Freedom.