
Baadhi ya Wajasiamali Wanawake Tanzania wakionyesha moja ya kazi za Uchoraji za Ujasiriamali kwa wageni waalikwa baada ya Chama cha Wanawake Wajasiriamali.
Akizungumza jijini mwanza katika maonesho ya wajasiriamali yanayofanyika viwanja vya jijini humo, mkurugenzi mtendaji wa Suvre Consultants LTD ya jijini Dar es salaam, respicious kundawa, amesema wajasiriamali wengi wanashindwa kurejesha mikopo yao mara wanapokopa kutokana na kutokuwa na elimu ya matumizi yake.
Amesema wamekuwa wakitoa elimu kwa wajasiriamali wengi baada ya kupata mikopo hususani vifaa kama mashine, lengo likiwa ni kuweza kutumia kwa uelewa na kurejesha dhamana wanayoweka.
Kundawa amesema wamekuwa wakitoa elimu ya masuala ya afya na usalama mahala pa kazi kwa wajasiriamali wa mikoa mbalimbali baada ya kupata mikopo kama mashine za aina tofauti.
Hata hivyo, kundawa amesema changamoto wanayokabiliana hivi sasa ni kukosekana vifaa vya kutolea elimu kwa wajasiriamali kwa baadhi ya mikoa likiwamo jiji la mwanza.
Awali mwenyekiti wa shirikisho la wafanyabiashara wa viwanda na kilimo ( (TCCIA) mkoa wa Mwanza, Lazaro Kihelya, amesema ni fursa pekee kwa wajasiriamali na wakulima kuwezeshwa kupatiwa mikopo toka kampuni ya Equity for Tanzania (EFTA), inayojishughulisha na shughuli hiyo kwa wajasiriamali na wakulima.