Wednesday , 10th Jan , 2018

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam, Ally Hapi amewataka wananchi waliojenga nyumba za na kuta katika maeneo ya mapitio ya maji kubomoa mara moja kabla manispaa haijabeba jukumu hilo litakalowagharimu.

Ally Hapi ametoa kauli hiyo alipokuwa kwenye ziara ndani ya wilaya yake, na kusema kitendo cha watu hao kujenga nyumba maeneo hayo kunasababisha maji kutopita kwenye mikondo yake na kufurika wakati wa mvua, hivyo watu hao ni vyema wakabomoa ili kuacha miundombinu ya maji salama.

Wananchi wanapenda kuilaumu serikali, lakini yapo baadhi ya maeneo uharibifu huu na adha hii ya maji unasababishwa na wao wananchi wenyewe, watu wanajenga wanblock njia za maji, mtu anajenga karibu na mtaro wa maji, matokeo yake maji yanakosa pa kupita yanajaa kwenye brabara zetu yanaingiakwenye nyumba za watu, na jambo la kusikitisha wataalamu wa ardhi wapo, wanapewa vibali, wanapewa hati, ni jambo la kusikitisha, sasa nataka kusema kwamba wananchi na wao wawe walinzi, wa mikondo na mikondo ya maji, ili sisi serikali tusiwe tunalaumiwa kila wakati", amesema Ally Hapi.

Mheshimiwa Hapi ameendelea kwa kusema kwamba wananchi watakaokaidi kufanya hivyo kwa muda watakaopewa, watabomolewa nyumba zao na manispaa hiyo na kwamba, watu hao watatakiwa kuilipa fidia na gharama za ubomoaji.