
Akizungumza kwenye Planet Bongo ya East Africa Television, Baraka amesema sababu inayomfanya yeye asifanye show nyingi ni kwa sababu anataka promoters wafikie ile pesa anayohitaji, ili kulinda brand yake.
"Mi nimiongoni mwa wasanii ambao nabagua sana show, mpaka nikifanya show mpaka promota afike bando ambalo nahitaji, na ninafaya hivyo ili kulinda brand yangu ambayo tayari nimeshaitengeneza, na kama nimeyumba kimaisha nayumba kweli kwa sababu maisha ndivyo yalivyo, kuna kupanda na kushuka, mpaka mataifa mkubwa wanayumba kiuchumi mimi ni nani, sio kitu kibaya, kinaweza kumtokea mtu yeyote", amesema Baraka The Prince.
Hivi karibuni kumekuwa na malalamiko kutoka kwa maashabiki kuwa msanii huyo sio tu amefulia, bali hata uwezo wake kwenye kazi umeshuka, na kushauri kama inawezekana awe anaandikiwa kazi zake.