Friday , 25th Jul , 2014

Wasanii kutoka Kenya, Kanjii Mbugua pamoja na A-star Richard kutoka Kenya, mwishoni mwa mwezi huu watafanya ziara ya kimuziki nchini Tanzania, ikiambatana na Kongamano litakaloangalia namna ya kutumia muziki na burudani kusaidia jamii.

mwanamuziki wa Kenya Kanjii Mbugua

Ziara hii itaanza tarehe 30 mwezi huu, mpaka tarehe 3 mwezi Agosti ambapo ikihusisha burudani kali jijini Dar es Salaam kutoka kwa Kanjii ambaye amejipanga kutumbuiza mashabiki kwa kazi safi kutoka albam yake mpya inayokwenda kwa jina Rauka, ikiwa na nyimbo 14 akiwa sambamba na A-star.

Kanjii na A-star ambao ni wakali katika sanaa ya ushairi, Hip Hop, Jazz na miondoko ya Afro Fushion wamejipatia umaarufu mkubwa kupitia maudhui ya sanaa yao ambayo hugusia masuala ya mahusiano, maisha na kifo kwa rika la vijana.