Thursday , 13th Mar , 2014

Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Mike ambaye anakuja kwa kasi katika miondoko ya R&B, ameachia video ya ngoma yake inayokwenda kwa jina Likizo, ambayo ndani yake amemshirikisha mkali wa michano kutoka Weusi, Rapa Joh Makini.

Mike amesema kuwa, hii ni kazi yake ya kwanza kabisa na tayari imempatia mafanikio makubwa na moyo wa kuendelea kufanya muziki, ambapo baada ya kufanya vizuri kupitia chati mbalimbali za Radio, anaamini kuwa video hii italeta mapinduzi katika TV.

Mike pia amesema kuwa, anajisikia faraja kutokana na sapoti ambayo amepata kwa rapa Joh Makini ambaye mbali na ratiba kali amempatia ushirikiano mpaka kazi hii imekamilia, na hapa tazama kionjo cha kazi hii.