Akizungumza na East Africa Readio, Mashali amesema, alitakiwa kukutana na Kalama mwaka jana lakini kwa bahati mbaya alipata ajali na kuambiwa kuwa anamkwepa Kalama suala ambalo kamwe hawezi kulifanya kwani anaamini na anauwezo wa kumpiga Nyilawila.
Mashali amesema, katika Pambano la mwisho alilokutana na Kalama walitoa sare suala ambalo bado lilionekana kuwa anamuogopa Mpinzani wake huyo.
Mashali amesema, anajiamini kwani aliweza kumpiga Bondia kutoka nchini Malawi hivyo pambano lake dhidi ya Kalama anaona halitakuwa na n agumu wa aina yoyote kwa upande wake kutokana na maandalizi anayoendelea nayo.