Lionel Messi
Kulingana na taarifa ya mwandishi wa habari, Juan Palo Varsky, aliyekuwa akiongea kwenye radio, moja nchini humo, Messi alifuatwa na watu watatu akiwa kwenye vyumba vya kubadilishia nguo, kabla ya mchezo baina ya Brazil na Argentina Novemba 11, mjini Belo Horizonte.
Watu hao waliomba awasaidie yeye kama Nahodha kulipwa mishahara ya miezi 6, wanayoidai kwa Chama Cha Soka nchini Argentina.
Messi, mwenye umri wa miaka 29, alitekeleza hilo suala kwa kuwasiliana na Baba yake, Jorge, na walinzi hao wakalipwa malimbikizo ya mishahara yao, baada ya chama cha soka nchini Argentina AFA, kukiri hakina fedha na kinadaiwa na wafanyakazi hao.
