.jpg?itok=zDgrbPvH×tamp=1472558422)
Akizungumza jijini Dar es salaam wakati wa kuzikabidhi Bendera timu za Uhamiaji, JKT Mbweni na JKT Ruvu, Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa BMT Dionis Malinzi kuwa amesema, timu hizo zinatakiwa kwenda kwa ajili ya kushindana na sio kushiriki ili kujihakikishia zinafanya vizuri katika mashindano hayo yanayoshirikisha nchi za Tanzania Bara, Zanzibar, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi.
Kwa upande wake kocha wa Timu ya Jkt Mbeni, Hafidhi Tindwa amesema, wanategemea kufanya vizuri katika m,ashindano hayo na kutokana na mazoezi wanaamini wataibuka na ushindi.
Kocha wa Jkt Ruvu, Argentina Daudi amesema, wanaamini nidhamu na mazoezi ya kutosha husaidia timu kuweza kufanya vizuri na kuweza kufika mbali zaidi na hatimaye kuibuka na ushindi, hivyo wanaamini nidhamu na mazoezi vitawasaidia kuweza kuipeperusha bendera ya Taifa katika michuano hiyo.
Kwa upande wa Kocha wa Uhamiaji, Mary Waya amesema, wanaamini watacheza kimataifa na hatimaye kuibuka na ushindi na pia kuzifanya timu nyingine shiriki katika michuano hiyo kuiga mfumo wao wa kucheza.