Saturday , 10th Jun , 2017

Hatua ya mtoano wa awamu ya kwanza michuano ya Sprite BBall Kings timu za Dream Chaser, Kurasini hits, The Fighter na TMT ndizo zilizong'ara leo dhidi ya wapinzani wao katika viwanja vya ukonga jijini Dar es salaam.

Timu za mashindano ya Sprite BBall Kings 2017 zikimenyana vilivyo

Katika michezo ya leo iliyohusisha timu nane ambazo ni mwendelezo wa mchujo utakaoweza kupata timu nane bora kati ya 18 za kushindania kitita cha shilingi milioni 15.

Dream Chaser (Blue) wakimenyana na Land Force (Nyeupe)

Katika hatua hiyo ya mtoano iliyoteka hisia za wapenzi wengi wa mpira wa kikapu wa jijini Dar es salaam  ilikuwa kama ifuatavyo kwa idadi ya vikapu ; Dream Chaser vikapu 92 huku Land force ikiambulia vikapu 72, Kurasini hit vikapu 142 Bongo hits vikapu 125, The Fighter ikiwa na vikapu 95 huku Chanika wakiondoka na vikapu 16 na Hatimaye TMT kuwaondoa Kwenye mashindano wapinzani wao God with us kwa vikapu 72-23.

Kurasini hits waliovaa njano, wenye jezi nyeupe ni Bongo hits 

Aidha katika timu zilizocheza leo wapo wafungaji  waliong'ara kwa kutupia vikapu vingi zaidi ambao ni Gwakisa Mwasakyeni wa timu ya Land Force '40', Yasin Choma wa timu ya Kurasini Hits 66, Chamundungwa wa The Fighter' 30 na Solomon Agrolous wa 'TMT' 27.

TMT na God with Us

Katika hatua nyingine, timu zilizoshinda leo zitalazimika kusubiri matokeo ya mechi za wiki ijayo ili ziweze kupimana kwa idadi ya magoli ili kupata timu 8 bora kati ya timu 18 za mzunguko wa mtoano wote kuwania kitita cha shilingi za kitanzania milioni 15 kutoka Sprite wakishirikiana na EATV.

The Fighter wenye jezi nyekundu na waliovaa nyeupe ni Chanika Legend 

Mchezo huo umechezeshwa na marefa  Shomari Athuman , Shabani Mohamed, Faraja Jima na Edwin Kilagwa.