
Mwenyekiti wa TRBA Ahmed Babla amesema, kumekuwa na viwanja vichache vya mchezo huo suala linalopelekea kukwamisha ndoto za baadhi ya wachezaji wanaochipukia kwenye mchezo huo.
Babla amesema, mchakato wa kutafuta amaeneo kwa ajili ya kuanza ujenzi wa viwanja hivyo unaendelea na sasa wanazunguka kwenda kukutana na maofisa wa michezo kuweza kuona namna ya kuanza ujenzi huo.
Babla amesema, lengo lao kubwa ni kuhakikisha wanaupeleka mchezo huo kwenye maeneo mbalimbali kwa kuhamasisha vijana kuupenda na kuuthamini mchezo huo kutokana na kuwa na hivi sasa michezo imekuwa ajira kubwa.