Tuesday , 26th Aug , 2014

TFF inaamini kutoa mafunzo kwa vijana katika kozi mbalimbali kutafungua milango ya nafasi za soka la kimataifa kwa wachezaji, waamuzi na makocha wa mchezo wa soka nchini,

Baadhi ya waamuzi na makocha vijana wanaohudhuria semina ya mafunzo ya FIFA kwaajili ya michuano ya Copa coca cola.

Shirikisho la soka nchini TFF wakishirikiana na shirikisho la vyama vya soka ulimwenguni FIFA na Afrika CAF pamoja na chama cha wamuzi Tanzania na chama cha makocha wameandaa semina maalum kwa ajili ya mafunzo ya makocha na waamuzi wa michuano ya copa coca cola ambayo inatarajiwa kuanza hivi karibuni hapa nchini

Ambapo ujumbe wa Fifa ukiongozwa na mkufunzi FelixTangawalima ulionyesha umeonesha a kuvutiwa zaidi na programu ya waamuzi chipukizi kuwekwa katika mafunzo hayo na kusema kuwa kama program kauli ambayo imeungwa mkono na mkurugenzi wa ufundi wa TFF ambaye ni mkufunzi wa FIFA Salum Madadi ambaye amesema mafunzo hayo yatasaidia kupunguza malalamiko hasa kwa waamuzi hapo baadae

Kozi hiyo inahusisha mafunzo kwa makocha 32 wa vijana na waamuzi 30 chipukizi ambao wameonesha uelewa wa hali ya juu kitu ambacho mgeni rasmi katika kozi hiyo katibu mkuu wa TFF Celestine Mwesigwa itakua ni chachu kwa soka hapa nchini na kwingineko Afrika Mashariki.