Rais wa FIFA Gianni Infantino
Mashindano hayo kwa sasa yanashirikisha timu 7, kutoka mabingwa wa mabara 6, wanachama wa FIFA, na timu moja ya nchi mwenyeji.
Rais wa Shirikisho la Soka Duniani FIFA, Gianni Infantino amesema kupeleka mashindano hayo, majira ya kiangazi kutavutia, wadhamini na watazamaji dunia nzima, na hivyo kutayapa mashindano hayo hadhi kubwa.
Mashindano ya Vilabu ya dunia, hufanyika kila mwaka katika mwezi wa Desemba, wakati ligi mbalimbali zikiendelea, na hivyo kupunguza watazamaji.
