Friday , 30th Jan , 2015

Mechi ya Ligi Daraja la kwanza kati ya Majimaji na Friends Rangers imeahirishwa baada ya kutokea vurugu Uwanjani.

Mechi hiyo iliyopigwa Mjini Songea,Majimaji walipata goli la kuongoza katika dakika za mwanzoni za kipindi cha kwanza na kuwafanya wapinzani wao kuhaha kutafuta goli la kusawazisha .

Katika dakika za mwisho za kipindi cha kwanza, Majimaji walipata Goli la pili lililopelekea wachezaji wa Friends Rangers kumsonga muamuzi, ambapo baada ya kuanza kwa vurugu hizo hivyo mchezo huo kuahirishwa.