Monday , 5th Jul , 2021

Unaweza kusema mambo bado yanamwendea kombo  Zari the Boss lady , baada ya kuripotiwa kuachana na aliyekuwa mpenzi wake ‘Dark Stallion’ ikiwa wamedumu kwa kipindi kisichopungua miezi 5 tu.

Picha ya Zari na aliyekuwa mpenzi wake

Zari amefuta picha zao kwenye ukurasa wake wa Instagram na kueleza kuwa ameumizwa na kuvunjika kwa mahusiano yao licha ya kuwa hayakumjenga kimaisha.

“I miss him, but I had to let him go. If it doesn’t build me I won’t keep it”.

The Boss lady na Mnigeria huyo waliweka wazi mahusiano yao mwezi Februari 14 mwaka huu ambayo huwa ni siku ya wapendanao.