Saturday , 28th Aug , 2021

Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa, amewajibu baadhi ya wananchi ambao wamekuwa wakilalamikia suala la kupanda kwa gharama za vifurushi, kwa kusema kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi tano Afrika ambazo gharama zake za vifurushi ziko chini ikilinganishwa na mataifa mengine.

Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa

Kauli hiyo ameitoia hii leo Agosti 28, 2021, Jijini Dodoma, wakati akizungumzia shughuli mbalimbali za utekelezaji wa miradi ya maendeleo nchini ikiwemo miradi ya kimkakati na masuala ya tozo na kodi.

"Ninafahamu kumekuwa na malalamiko ya vifurushi vimepanda, lakini niwaambie gharama za bando kwa Tanzania sisi ni kati ya nchi 5 Afrika zenye gharama za chini za vifurushi, ziko baadhi ya nchi za Ulaya na Amerika ambazo gharama zake ni kubwa, ninafahamu iko nchi sitataja jina ambayo unanunua GB 1 kwa Dola 15 lakini hapa wananchi wanapata GB 1 kwa chini ya 2,000," amesema Msemaji Mkuu wa Serikali