Monday , 6th Sep , 2021

Mwandishi wa Habari wa Azam Media, mkoa wa Kagera Nicolaus Ngaiza, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Septemba 6, 2021, badaa ya gari walilokuwa wakisafiria kutoka wilaya ya Biharamulo walipokwenda kikazi kupata ajali katika eneo la Gwanseli wilayani Muleba.

Mwandishi wa Habari wa Azam Media, mkoa wa Kagera Nicolaus Ngaiza, wakati wauhai wake

Katika ajali hiyo pia mwandishi wa habari wa Clouds Media Group Benson Eustace, alikuwemo na amejeruhiwa na amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Kagera wodi namba nne akiendelea kupatiwa matibabu.

Ajali hiyo imetokea wakati wakiwa njiani kurudi Bukoba. Taarifa kamili zitatolewa baadae.