
Kushoto ni Waziri Dkt Dorothy Gwajima akiwa na mtoto aliyekuwa akimuuguza Bibi yake na kulia ni Spika wa Bunge Job Ndugai.
Spika Ndugai ameitoa kauli hiyo leo Septemba 6, 2021, Bungeni Dodoma.
"Nakushukuru sana Mh. Waziri kwa kufika Mwanza kwa yule binti wa miaka 9 na tunashukuru kwa hatua ambazo mmezichukua ni stori inayosikitisha sana," amesema Spika Ndugai.
Hivi karibuni iliripotiwa taarifa ya mtoto wa miaka 9 anayemhudumia Bibi yake ambaye ni mgonjwa hali iliyopelekea kukosa masomo huku wazazi wake nao wakiwa hawajawahi kumtafuta tangu alipoenda Mwanza kumsalimia Bibi yake huyo akitokea Zanzibar, ambapo mara baada ya taarifa hiyo Waziri Gwajima alienda Mwanza na kusaidia mtoto huyo kurudi tena shule.