
Kocha wa Tottenham Hotspurs, Nuno Espirito
Mwenyekiti wa Tottenham Hotspurs, Daniel Levy amekutana na Mkurugenzi wa soka Fabio Paraciti kujadili mwenendo wa Kocha huyo.
Kocha huyo wa zamani wa Wolves alisaini Mkataba wa miaka miwili wa kuifundisha Tottenham Hotspurs mnamo mwezi Juni mwaka huu.
Licha ya kuanza vizuri msimu, Spurs imepoteza mechi tano kati ya saba za Ligi Kuu ya Ungereza, wakikamata nafasi ya nane kwenye msimamo wakiwa nyuma kwa alama kumi dhidi ya vinara Chelsea.
Iwapo Levy atafanya maamuzi, huenda aliyekuwa kocha wa AS Roma, Paulo Fonseca ambaye amekuwa akiwindwa kwa muda mrefu na klabu hiyo.