Thursday , 16th Dec , 2021

Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp hanampango wakufanya usajili wa wachezaji watakaoziba nafasi za wachezaji Mo Salah na Sadio Mane watakao kosekana kwa takribani mwezi mzima kutokana na ushiriki wao kwenye michuano ya mataifa barani Afrika AFCON inayoanza January 9 mpaka Februari 6, 2022.

Jurgen Klopp kulia akiwa na Sadio Mane katika na Mo Salah kushoto

Klopp atawakosa wachezaji watatu Sadio Mane ambaye atakuwa na kikosi cha timu ya taifa ya Senegal, Mo Salah na kikosi cha timu ya taifa ya Misri na Naby Keita ambaye ni raia wa Guinea na timu zao zitakuwa zikiminyana kwenye michuano hiyo ya mataifa barani Afrika itakayofanyika nchini Cameroon.

Kuhusu kuwakosa wachezaji hao Kocha klopp amesema anafuraha na kikosi alichonacho hivyo hatafanya usajili,

"Tulijua wachezaji watatu wangefuzu na tulijua kwamba angalau wawili kati yao watafika mbali sana kwenye hayo mashindano. Je, unaweza kuwa tayari kwa kitu kama hicho, vizuri, kikamilifu? upate mbadala wa kila mmoja, mbadala wa Sadio, mbadala wa Mo, mbadala wa Naby? Hilo ni gumu katika kila hali lakini nina furaha na kikosi nilichonacho tunawachezaji na bado tutaendelea kucheza soka. Tuna imani kabisa tutapata suluhu.'' amesema Klopp kocha wa Liverpool

Lakini pia kumekuwa na mashaka juu ya kufanyika kwa michuano ya AFCON kutokana na mlipuko wa kirusi kipya cha Uviko 19 (Omicron) ingawa waandaaji wa michuano hiyo kamati ya mashinda ya nchini Cameroon ambao ni wenyeji pamoja na Shirikisho la Soka barani Afrika CAF wamethibitisha kuwa mashindano hayo yatafanyika kama ilivyopangwa.

Mane na Salah ni wachezajai muhimu kwenye kikosi cha Liverpool msimu huu tayari Mo Salah ameshafunga mabao 21 kwenye michuano yote akiwa ndio kinara wa ufungaji kwenye kikosi hicho, wakati Mane ni mfungaji wa pili akiwa na mabao 9 kwenye michuano yote.