
Simba wanatinga hatua hii baada ya kuifunga Red Arrows kwa jumla ya magoli 4-2 na kujihakikishia ushiriki na uwakilishi wa Tanzania kwenye mashindano kimataifa kwa mara ya nne ndani ya miaka mitano iliyopita.
Kwenye upangaji wa makundi Simba wapo kwenye chungu nambari mbili wakiwa pamoja na CS SFaxien ya Tunisia, Orlando Pirates ya South Africa na Coton Sport ya Cameroon.
Chungu nambari moja wapo mabingwa mara tano wa Ligi ya Mabingwa barani Afrika, TP Mazembe ya DR Congo, matajiri wa Cairo, Pryamids FC ya Misri, RS Berkane ya Morocco na huku JS Kabylie na Royal Leopards wakiwa bado hawajui hatma yao ya nani atasonga mbele kutokana na kutocheza mchezo wa marudiano.
Al Masry, Zanaco FC, JS Saoura and ASEC Mimosas wapo chungu cha tatu, na chungu cha nne kikihitimishwa na AS Otoho d'Oyo, Al Ahli Tripoli, Al Ittihadi SC na US Gendarmie.
Katika hatua ya upangaji wa makundi timu moja itakutoka kwenye kila chungu na kufikisha idadi ya makundi manne kama utaratibu ulivyo.