Wednesday , 29th Dec , 2021

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, amesema kwamba wajibu wa serikali ni kuhakikisha watoto wote wanakwenda shule na kuondoa kabisa tabia ya kukuta watoto wakifanya biashara kwenye stendi za mabasi au nyumba za starehe.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa

Waziri Mkuu amesema kwamba jukumu la kulea watoto na kutafuta mahitaji ni la wazazi lakini wajibu wa kuwasomesha watoto hao ni wa serikali.

“Tulishasema, mtoto wa Kitanzania kwenda shule ni lazima, watoto ni wao, lakini kwenda shule ni lazima, ndiyo maana serikali ilifuta ada katika shule zote," amesema Waziri Mkuu