Wednesday , 5th Jan , 2022

Joel Embiid wa Philadelphia 76ers na Donovan Mitchell wa Utah Jazz wameibuka kuwa washindi wa tuzo za mchezaji bora wa Ligi ya kikapu nchini Marekani ‘NBA’ kwa mwezi Disemba 2021 baada ya kuonesha viwango bora.

(Donovan Mitchell wa Utah Jazz (kushoto) na Joel Embiid wa Philadelphia 76ers)

Katika michezo ya mwezi huo, Embiid alikuwa na wastani wa kufunga alama 29.2, rebound 11.2 na Assist 3.9 zilizoisaidia timu yake ya Philadelphia 76ers kupata ushindi kwenye michezo 8, kufungwa 2 katika michezo 14.

Kwa upande wa Donovan Mitchell, yeye alikuwa na wastani wa kufunga alama 30.2, rebound 11.2 na Assist 3.9 zilizoisaidia timu yake ya Utah Jazz kupata ushindi kwenye michezo 12 kati ya 14 na kufungwa 2 pekee.

Joel Embiid ni mchezaji bora wa NBA mwezi Diemba kwa mwezi Disemba kutoka ukanda wa Mashariki ‘Eastern Conference’ ilhali Donovan Mitchell ni bora kwa mwezi huo kwa ukanda wa Magharibi ‘Western Conference’.

Michezo ya NBA iliendelea tena alfajiri ya kuamkia leo kwa michezo mitano ambapo Cleveland Cavaliers 106-110  Mamphis Grizzlies, Toronto Raptors129-104 San Antonio Spurs, New York Knicks 104-94 Indiana Pacers, New Orleans Pelicans 110-123 Phoenix Suns na Los Angeles Lakers 122-114 Sacramento Kings.