
Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika,Tawi la Tanzania MISA – TAN, Bi. Salome Kitomari
Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika,Tawi la Tanzania MISA – TAN, Bi. Salome Kitomari wakati akizungumza kwenye maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari leo Jumanne Mei 3 ,2022 amesema MISA-TANZANIA inampongeza Rais Samia Suluhu kwa kazi nzuri anayoifanya ya kututumikia Watanzania huku ikiahidi ushirikiano katika ujenzi wa taifa Tanzania.
“Tangu umeingia madarakani Machi,mwaka 2021,tumeona mabadiliko chanya ya ukuaji wa sekta ya habari nchini,tunaona uhuru wa kujieleza,upatikanaji wa taarifa na vyombo vya habari unazidi kuongezeka siku hadi siku na tumeshuhudia vyombo vya habari vilivyokuwa kifungoni vimefuguliwa.
Tunatarajia serikali yako itaendelea kusaidia ukuaji wa sekta ya habari,ikiwamo kuendelea kujenga mazingira mazuri na wezeshi kwa wafanyabiashara au waliowekeza kwenye vyombo vya habari ili waweze kutoa maslahi mazuri kwa wanahabari”, amesema Kitomari.