Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Malori yanayosafirisha bidhaa kwenda Kenya yakwama

Saturday , 14th May , 2022

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, amesema kuwa Serikali itawasiliana na Mamlaka za Kenya ili kutatua changamoto ya malori ya mizigo yanayovuka kupeleka bidhaa nchini humo kutumia muda mrefu kupata vibali vya kuvuka mpaka wa Horohoro-kuingia Kenya

Dkt. Nchemba alisema hayo baada ya kuzungumza na madereva wa malori yanayobeba shehena ya mizigo kwenda Kenya katika Mpaka wa Horohoro, akiwa njiani kwenda Mombasa-Kenya, kwenye Mkutano wa Mawaziri wa Fedha wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Madereva hao walieleza kuwa wanapata usumbufu mkubwa kwa sababu wanatumia muda mrefu unaokadiriwa kufikia hadi siku 14 hadi 21 kuvuka mpaka wa Horohoro kwenda nchini Kenya, wakati upande wa madereva wa Kenya wanaoingia Tanzania wanatumia siku zisizozidi 3 kuvuka mpaka huo.

Walimweleza Dkt. Nchemba kwamba, kuchelewa kuvuka mpaka kunawaletea matatizo makubwa ikiwemo kutumia gharama kubwa zisizolingana na posho za safari wanazopewa na waajiri wao, lakini pia kuna baadhi ya bidhaa zinaharibika kabla ya kuvuka mpaka.

Dkt. Nchemba alisema amebaini kuwa ucheleshwaji wa huduma ya forodha kwa Kenya unatokana na nchi hiyo kutoanza kutumia  Mfumo wa Pamoja wa Huduma ya Forodha (Single Custom Territory) kama walivyokubaliana.

Alisema kuwa magari ya Kenya hayapati changamoto hiyo ya foleni kwa kuwa Tayari Tanzania wanatumia mfumo huo ambapo mizigo yote ya Kenya hupata vibali ikiwa huko huko nchini Kenya, kabla ya kufika katika mpaka huo wa Horohoro na malori kupita bila tatizo.

Dkt. Nchemba alisema kuwa atawasiliana na Waziri mwenzake wa Fedha wa Kenya ili kuanza kutekeleza makubaliano ya kuweka Mfumo huo wa Pamoja na Forodha kwa kuwapeleka watumishi wa nchi hiyo upande wa Tanzania ili kuharakisha usafiri na usafirishaji wa mizigo kutoka Tanzania hivyo kuwaondolea adha wafanyabiashara na madereva wanaotumia mpaka huo kufanya biashara zao.

HABARI ZAIDI

DCP David Misime, Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania

Mtoto atekwa na mzazi wake ili ajipatie milioni 20

Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Anton Sabasaba Akizungumza wakati alipohudhuria kikao cha wazazi katika Shule ya Msingi Elisabane Mei 24, 2024

Wototo wafuatiliwe na kulindwa kama mboni - Anton

Maduka ya Wafanyabiashara yakiwa yamefungwa

Wamiliki wa maduka Mebya wafunga biashara zao

Kamanda wa Polisi mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Agustino Senga

Polisi waambiwa kazi yao ni kazi ya Mungu

Kiwanda cha sukari Mtibwa

11 wafariki dunia kiwanda cha Mtibwa

Wilman Kapenjama Ndile, Mkuu wa Wilaya ya Songea

DC Kapenjama ataka uaminifu kwa wakulima Songea

Bashiri Mohamed (35) Mwenye Koti Jeusi akiwa anafikishwa Mahakamani Ilemela, Jijini Mwanza

Aliyezini na binti yake apandishwa kizimbani