Thursday , 19th May , 2022

The African Boy Juman Jux na mrembo Huddah The Bosschick kutoka 254 Kenya wamezidi kuwaacha mashabiki midomo wazi mitandaoni kuhusu madai ya wawili hao kuzama penzini.

Picha ya Juma Jux na Huddah

Jux amemtumia Huddah kama 'Video Queen' wa ngoma yake ya simuachi ambapo ameonekana kumkiss mdomoni jambo ambalo linasemekana limeongeza madai ya wawili hao kuwa ni wapenzi.

Hii sio mara ya kwanza kwa Jux kuhusishwa kuwa kwenye mahusiano na Huddah, story hizo zilianza baada ya Jux kuachana na Vanessa Mdee.