
Aidha Naibu Waziri amesema watumishi nchini wana deni kubwa kwa Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan
" Watumishi wa umma tuna deni kubwa kwa Rais wetu Samia Suluhu Hassan, tayari yeye ameonesha kwa vitendo kuwajali watumishi ambapo ameongeza mshahara kwa asilimia 23 kama hiyo haitoshi tayari ametoa kibali cha kuongeza posho za watumishi, tumlipe Rais wetu kwa kufanya kazi kwa bidii,"
"Jambo lingine ni kuongeza ubunifu kazini, epukeni kuwa walewale kila siku, Kanuni na taratibu za Utumishi wa Umma ziko wazi lakini hatumzuii mtu kuonesha kipaji chake na kuwa mbunifu ili kuongeza ubora wa kazi zake,"amesisitiza Naibu Waziri Ndejembi.