Tuesday , 31st May , 2022

Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Duniani WHO zinaonyesha utumiaji wa bidhaa za Tumbaku husababisha vifo kwa karibu nusu ya watumiaji wake na zaidi ya watu takribani Milioni 8 hufariki kila mwaka kutokana na matumizi ya Tumbaku.

Takwimu hizo zimetolewa leo Jijini Dodoma na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ikiwa leo Tanzania imeungana na nchi nyingine Duniani kuadhimisha siku ya kutotumia Tumbaku Duniani ambayo hufanyika kila tarehe 31 Mei ya kila mwaka.

Waziri Ummy amesema waathirika wengi wa matumizi ya Tumbaku wanatokea katika nchi zinazoendelea ukilinganisha na nchi zilizoendelea.