
Sadio Mane
Awali Bayern Munich waliripotiwa kupeleka Ofa ya pesa za Ulaya Euro Milion 30 ambayo ni zaidi ya Bilioni 74 kwa pesa za Tanzania (74,982,670,404.81) kama ada ya uhamisho ya mchezaji huyo, mabingwa hao wa Ujerumani wakaboresha tena offa yao kwa kupeleka tena dau la Euro milioni 35 ambayo ni sawa na Bilioni 87,473,097,250.55 kwa pesa za Tanzania lakini Liverpool wameikataa offa hiyo.
Kwa mujibu wa ripoti Liverpool wanataka dau la Euro million 50 kama ada ya uhamisho ya msahmbuliaji huyo raia wa Senegal mwenye umri wa miaka 30, klabu hiyo ikarudi tena na Offa ya Euro Milion 35 ambayo nayo imekataliwa huku taarifa zikidai kuwa Liverpool wanataka walau dau la Euro milion 50 sawa na billioni 124,929,743,464.63 kwa pesa za Tanzania.
Mkataba wa Mane ndani ya kikosi cha Liverpool unamalizika mwezi Juni mwakani 2023. Na mshambuliaji huyo mara kadhaa ameonyesha nia yakutaka kuondoka katika klabu hiyo. Bayern wanamuwania Mane kama mbadala wa Robert Lewandowski ambae ameomba kuondoka akihusishwa kujiunga na FC Barcelona ya Hispania.