
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan
Taarifa ya Ikulu iliyotolewa usiku wa kuamkia leo Julai 28, 2022 imeeleza kuwa Rais Samia amemteua Albert Chalamila kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera. Chalamila amewahi kuwa Mkuu wa mkoa wa Mbeya na Mwanza.
Aidha Rais Samia amemteua Dk. Yahaya Nawanda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu akichukua nafasi ya David Kafulila. Kabla ya uteuzi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Tabora.
Pia Rais Samia amemteua Dk. Raphael Chegeni kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara akichukua nafasi ya Ally Hapi.
Soma taarifa kamili hapo chini.