Tuesday , 4th Oct , 2022

Vijiji kumi na mbili  katika halmashauri ya Mtwara vinatarajiwa kupitishwa  bomba la gesi  asilia la lenye urefu wa kilomita 35

Wananchi  wa vijiji hivyo wametakiwa kutoa ushirikiano kwa shirika la  maendeleo ya petroli  Tanzania, (TPDC) kwa ajili ya kufanya tathimini  ya mali, na  kulipwa fidia zao, kwa ajili ya kuanza utekelezaji  mradi huo.

Akizungumza  na wananchi wa Kijiji cha  Moma  kata ya Moma  katika kutambulisha mradi huo Mkuu wilaya ya  hiyo Dustan Kyobya,  akawataka wananchi kupokea mradi huo na kutoa ushirikiano wa kutosha wakati wa zoezi hilo