
Kwa mujibu wa utafiti uliowezeshwa na Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi wa Nchi za Pembe ya Afrika Igad, endapo mvua hazitanyesha za kutosha hali itakua mbaya zaidi.
Mkurugenzi mtendaji wa Igad,Workneh Gebeyehu,amesema kwamba migogoro inayolikumba eneo la ukanda huo imechochea ukosefu wa chakula na kuongeza hatari ya njaa.
Pia ametaka mashirika ya kimataifa kusaidia jumuiya za Afrika Mashariki ambazo zinapitia wakati mgumu wa ukame kuwahi kutokea ndani ya miaka 40 iliyopita.