Sunday , 9th Oct , 2022

Wazee na walemavu wanaoishi katika nyumba maalumu kwaajili ya kutunzwa katika eneo la Lasibula Mkoani Lindi, wamewaomba wadau mbalimbali wawasaidie kurekebisha nyumba yao ambayo kwasasa ni chakavu huku wakiwasihi kuwakumbuka mara kadhaa pale wapatapo nafasi

Wazee wa eneo la Lasibula Mkoani Lindi

Wakizungumza na EATV baada ya kutembelewa na wadau kutoka shirika la posta mkoani Lindi, ambao katika kuadhimisha siku ya Posta duniani wamewatembelea wazee hawa kuwajulia hali na kuwapati zawadi.

Wazee hawa wameieleza changamoto hii na zinginezo nyingi kama suala la kukosa madawa ya dharula kituoni hapo huku wakiliomba shirika hilo liwasaidie kupaza sauti kwa wadau , kwani jumba lao chakavu na bati zinazovuja ni suala linalowasumbua hasa katika misimu ya mvua na suala la dawa ni muhimu kwa afya zao kwani kutokana na umri wao kusogea,,,huumwa mara kwa mara.