Tuesday , 11th Oct , 2022

Watu watano wamefariki dunia na wengine 26 kujeruhiwa, baada ya gari ndogo ya abiria aina ya Toyota Coaster, iliyokuwa ikisafirisha maiti kugongana uso kwa uso na Basi la abiria la Kampuni ya Kyela Express, wilayani Rungwe, mkoani Mbeya.

Ajali Rungwe Mbeya

Kwa mujibu wa Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Dk Vincent Anney, ajali hiyo imetokea leo Oktoba 11, 2022 majira ya asubuhi katika kitongoji cha Kanyegere, Kijiji cha Ibula, Kata ya Kiwira, Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya.

Dk Anney amesema kwamba, miongoni mwa watu waliopoteza maisha ni pamoja na dereva wa Coaster iliyokuwa ikisafirisha maiti kutoka Dodoma, kwenda Kyela.