Tuesday , 11th Oct , 2022

Mama mwenye umri wa miaka 35 na mtoto wake wa miezi 10, wamepoteza maisha baada ya kukanyagwa na gari wakiwa kwenye bodaboda eneo la mtaa wa Nguzo Nane, Manispaa ya Shinyanga akitokea Morogoro kufuata vyeti vyake Chuo Kikuu cha Mzumbe huku mwendesha bodaboda akitokomea kusikojulikana.

Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga

Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa hospitali ya Rufaa mkoa wa Shinyanga Daktari Luzila John, amesema wamepokea mwili wa mwanamke huyo ambaye alipoteza maisha katika eneo la ajali na mtoto wake alifariki baadaye wakati akipatiwa matibabu.